Wednesday, November 30, 2011

SIKU YA UKIMWI DUNIAN:KNOWING IS NOT DOING

Socrates kama mshauri mkubwa wa mambo ya hekima na busara Duniani, alikuwa mwepesi wa kutoa majibu ya matatizo sugu yaliyokuwa yakiisumbua Dunia enzi zake. Kwa mfano yeye anasema kabisa knowledge tu kwa mtu haitoshi na wala haiwezi kumsaidia kabisa endapo hataitrasnform katika uhalisia. Point ya huyu Mzee ni kwamba unaweza kuwa unafahamu mambo mengi sana ila bado ukaendelea kubaki kuwa mpumbavu. Hebu tuangalie kama ya huyu mbabu yanaukweli au vipi.Kipindi gonjwa la UKIMWI limeingia kijijini kwetu (Kibondo Kigoma) watu walisema ni gonjwa la mjini na waliokuwa wanakufa kweli walitoka mjini. Huko kwetu kipindi hicho kwenda mjini ilibidi uwe msomi au mfanyabiashara(Mwalimu ndo alikuwa msomi mkubwa akifatiwa na mwanajeshi). Hii ilipelekea nijiulize maswali mengi sana pasipokupata majibu. Mungu saidia shuleni nikafundishwa  kuwa gonjwa hili ni Upungufu wa Kinga Mwilini na halikuwa gonjwa la watu wa mjini tu.Karibu kila nyanja ya elimu likaanza kufundishwa kwa kasi sana. Nakumbuka kipindi namaliza kidato cha nne ndo moja ya maswali katika BIOLOGY nililojibu kwa kujiachia kabisa. Mpaka leo hii naongea sidhani kama kunamtanzania asiyejua undani wa gonjwa hili . We know a lot brothers and sisters about UKIMWI. Mtu usipokuwa na fikra pevu kama Socrates unaweza kushangaa kwa nini gonjwa la UKIMWI limesambaa sana hasa kwa wasomi wenye mpaka shahada za uzamifu ambao wanajua scientific courses and effects of HIV/AIDS?Jibu ni rahisi sana. Knowing is not doing.

Ngoja nikuchekkeshekidogo. Pale kwetu kibondo miaka ya 2000 kulikuwa na daktari bingwa wa upasuaji BUT alikuwa anafanya kazi hii nzuri ya kuokoa maisha ya watu baada ya kunywa GONGO na kulewa chakali na sigara mkononi. La ajabu ni huyuhuyu daktari alikuwa akija shuleni  na kutufundisha madhrara ya kunywa pombe na sigara katika afya ya binadamu. Alitwambia unapokunywa gongo na kuvuta sigara utauunguza mapafu. Mbona yeye alikuwa akivuta na kunywa? KNOWING IS NOT DOING.

Nachotaka kukwambia KUJUA ni kitu kimoja  na KUTENDA ni kitu kingine na kwa pamoja ndo humuumba MSOMI

1 comment:

PARENTS said...

Its kinda ironic ila ndio ukweli wenyewe wa mambo katika dunia ya leo.
Kikubwa hapa ni kauli ya waleo wasemao kuwa "Gonjwa hili limewekwa pabaya"...japo ni kujiendekeza kuamini hivyo ila ni wazi kuwa haifai kuelekeza nguvu katika kuujua ukimwi na madhara yake bali namna ya kukabiliaa na chanzo chake...tamaa za mwili, kutokujali, sifa, pombe na vitu vinginevyo!!

Umeanza na mheshimiwa Socrates, ni kweli kabisa asemacho, bila shaka aliendelea zaidi ya hapo..kwamba nii kifanyike na kwa namna gani kitafanikiwa...tafadhali bwana muandishi usituache hivi bali uendelee alipoendelea.